Zaidi ya Wanawake 260 walibakwa wakati wa jaribio la kutoroka kwa Wafungwa kutoka Gereza la Kati la Makala Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mapema mwezi huu, kwa mujibu wa ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa.
Walau Watu 129 waliuawa wakati Walinzi wa Gereza walipotumia Risasi dhidi ya Wafungwa waliokuwa wakijaribu kutoroka, Gereza hilo, ambalo lina uwezo wa kuchukua Wafungwa 1,500, lilikuwa na zaidi ya Watu 15,000 wakati wa tukio hilo na Serikali ilikuwa imethibitisha kwamba kulikuwa na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, lakini haikutoa idadi maalum.
Ripoti ya UN ilibainisha kuwa kati ya Wanawake 348 waliokuwepo Gerezani, 268 walipitia unyanyasaji wa kijinsia, wakiwemo Wasichana 17 walio chini ya umri wa miaka 19.
Waathirika walihitaji msaada wa haraka ikiwa ni pamoja na Dawa za kinga baada ya shambulio ndani ya saa 72.
Aidha Shuhuda mmoja alielezea kwa hofu jinsi Wafungwa wa kiume walivyovamia Wanawake, huku Wanawake wazee nao wakipitia unyanyasaji huo, hadi sasa, Rais Felix Tshisekedi ameagiza uchunguzi juu ya tukio hilo na kutaka ukaguzi wa Magereza makuu Nchini ili kupunguza msongamano wa Wafungwa, hakuna mafanikio ya kutoroka yaliyotokea licha ya vurugu hizo.