Mkaguzi kata ya Ngara Mjini Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/Insp Olipa Chitongo amekutana na wahitimu wa Shule ya Msingi Nyabihanga Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera na kuwapa Elimu na mbinu ya kuepuka vishawishi mara baada ya kuhitimu elimu yao ya Msingi.
Mkaguzi huyo ametoa elimu hiyo kwa wahitimu hao huku akiwataka kuto kukubali kuwashawishiwa na watu ambapo amebainisha kuwa wakikubali ushawishi wa watu katika masuala ya mahusiano ya kimapenzi watapoteza ndoto zao za baadae ikiwa nipamoja na maendeleo yakielimu.
Aidha Mkaguzi Chitogo amewaambia vijana hao kuwa bado wanasafari ndefu katika masomo huku akiwataka kutambua kuwa hatua hiyo ni mwanzo kabsa katika safari yao ya kimasomo.
Vilevile amewataka kutumia vizuri muda wa kusubili matokeo kwa kujiongezea ujuzi katika kozi za muda mfupi ili ziwataisaidie baada ya kufaulu na kuendelea na masomo yao ya Sekondari.
Sambamba na hayo amewaomba wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri katika kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Juu ya wahalifu na uhalifu katika Maeneo yao.