Kampuni ya GSM kupitia Mall yake inayopatikana Msasani Dar es salaam ( pembenji ya Ubalozi wa Marekani) imetangaza kitu kipya kinaitwa MIDNIGHT SALE ambalo ni punguzo kubwa la bei ya bidhaa mbalimbali katika Mall hiyo ambayo kuanzia leo Ijumaa September 13 hadi Jumapili September 15 mall hiyo itakuwa wazi hadi saa sita usiku ili kila mmoja apate muda mzuri wa kusomba vitu katika SALE hiyo.
Vanessa Ruhuza, Mwakilishi wa Kampuni ya GSM amesema GSM Mall hufungwa kila siku saa tatu usiku lakini kuanzia leo hadi Jumapili itafungwa saa sita usiku “tunataka kuwafikia Watu wanaoshindwa kufika katika maduka yetu mapema lakini tumeona tuwape ofa ya kuelekea kipindi cha MAULID, pia Wateja wataofika katika muda huo watapatiwa maji ya bura ya GSM pembeni ya vitafunwa vitakavyokuwepo”
Pia Vanessa amesisitiza kuhusu ujio mpya wa kitu kinaitwa GSM REWARDS ambayo itamuwezesha Mteja yeyote kusajiliwa na kujikusanyia points kila anapofanya manunuzi, points ambazo zitampunguzia bei au gharama katika shopping zijazo.