Taarifa zinasema kuwa Donald Trump yuko salama baada ya risasi kurushwa “karibu naye”, timu yake ya kampeni imetangaza siku ya Jumapili Septemba 15, 2024, miezi miwili baada ya jaribio la mauaji ambalo lilimlenga mgombea huyo wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais wa Marekani.
Rais huyo wa zamani wa Marekani alikuwa katika klabu yake ya gofu huko Florida kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
“Yuko salama salimini baada ya risasi kufyatuliwa karibu naye,” Steven Cheung, mkurugenzi wa mawasiliano wa kampeni ya Donald Trump, amesema katika taarifa, na kuongeza kuwa “hakuna maelezo zaidi kwa sasa.”
Mnamo Julai 13, mkuu wa mali isiyohamishika, na mgombea wa Republican katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba, alijeruhiwa katika sikio kwa risasi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili kujeruhiwa miongoni mwa watu waliokuwa wakifuata na kusikiliza mkutano wake wa kampeni huko Pennsylvania, kaskazini mashariki mwa nchi.
Picha za Donald Trump, damu zikitiririka usoni mwake, huku akiinua mkono wake, zilizunguka ulimwengu mzima.
Mhusika wa shambulio hilo aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.