Joe Biden anapanga kuzuru Angola kabla ya uchaguzi wa urais wa Novemba 5. Hivyo atakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Afrika tangu Barack Obama mwaka 2015. Ziara hiyo bado inakamilishwa, lakini itakuwa ni uthibitisho zaidi kwamba Washington inatafuta kurekebisha uhusiano wake na Afrika.
Ikulu ya White House kwa sasa inakataa kutoa maoni juu ya ziara iliyopangwa ya Joe Biden kwenda Angola, lakini vyombo vya habari vya Marekani tayari vinazungumza juu zira hiyo, haswa, kwa sababu ziara hii ilikuwa kwenye kalenda. Ziara hii iliyopangwa mwaka jana, iliahirishwa baada ya kuzuka kwa vita kati ya Israel na Hamas.
Akiwa bado mgombea katika uchaguzi wa urais wa Marekani, Joe Biden alitangaza mwezi Mei 2024 kwamba angeenda Afrika mwezi Februari 2025 ikiwa ataibuka mshindi katika uchaguzi huo. Kujiondoa kwake kwenye kampeni kunamruhusu kufanya ziara hii mapema kuliko ilivyopangwa.