Wakala wa mabasi yaendayo haraka Dart wamesema wapo tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwa makampuni ya kichina yanayojenga mradi huo awamu ya nne unaotoka Posta hadi eneo la Boko Basihaya Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mualiko maalum kutoka kwa Mkandarasi wa Karakana kwa ajili ya mradi huo Kampuni ya China Communication Construction Company (Mid Autumn Festival) Afisa Mipango na usafirishaji wa Dart Nason Bwatuta amesema kwa kujumuika pamoja na Mkandarasi huyo kutawajengea uwezo na mawanda mapana ya namna bora ya kujenga na kushirikiana katika mradi huo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni inayojenga karakana katika mradi huo ya China Communication Construction Company (CCCC) Gou Xudong amesema upio umuhimu mkubwa wa kukutana na wadau wa miradi mbalimbali kwa lengo la kubadilishana uzoefu tamaduni na masuala mengine yatakayoleta wepesi katika majenzi.
Tafrija hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo jumla ya Kampuni tatu za Kichina zimekabidhiwa mradi huo wa DART IKIWEMO CCCC ili kuharakisha kukamilika kwake ambapo itasaidia kurahisisha shughuli za ukuaji wa uchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.