Safu za Milima ya Uluguru ikiteketea Kwa moto Kwa zaidi ya siku Saba tangu septemba 10 mwaka huu huku chanzo kikitajwa kuwa ni wakulima na wawindaji kuchoma mashamba kwa ajili ya maandalizi ya Kilimo pamoja Imani potofu Kwa wananchi kuwa akichoma moto ukienea eneo kubwa siku zake za kuishi bado ni nyingi.
Mhifadhi mkuu hifadhi ya mazingira asilia Uluguru Benadetha Chile amesema Kwa Sasa wanashirikiana na Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa Morogoro na wanachi wa eneo hilo kuthibiti moto huo.
Anasema changamoto ya safu hizo kuteketea kwa moto ni za Kila mwaka Kila msimu wa Kilimo unapoanza hivyo jitihada mbalimbali za kutoa elimu zinafanyika kushirikisha wanachi hao.
Amesema licha ya wakulima, wawindaji kuwa chanzo cha moto huo lakini pia kumekuwa na Imani potofu Kwa wananchi hao kuchoma.moto hovyo na endapo moshi utaenda juu zaidi na moto kusambaaa eneo kubwa basi anajua umri wake wa kuishi bado ni mrefu.