Jumla ya Sh bilioni 67 zimezalishwa na wakulima wa Tumbaku katika Halmashauri ya Manispaa ya Ushetu kutoka katika bero 204,329.10 ambayo ni sawa na Kilogramu milioni 10 zilizozalishwa na wakulima hao.
Hayo yameelezwa leo Septemba .., 2024 na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani alipokuwa akizungumza na wakulima wa halmashauri hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Waziri wa Kilimo, Hussein Muhamed Bashe.
Aidha, Cherehani alieleza licha ya kazi kubwa inayofanyika bado mzigo wa madeni umekuwa kwa wakulima, hivyo aliiomba wizara kusaidia wakulima kuondokana na madeni hayo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Umefanya mengi kwenye korosho, umefanya mengi kwenye Pamba, umefanya mengi kwenye chai fanya tena kwenye chai fanya jingine kwenye tumvaku mzigo wa miti wakashughulikie wanunuzi wa tumbaku kwa gharama zao sio kwa gharama za wakulima,” amesema Cherehani.