Viongozi Wanawake wa Vyama vya siasa wamezungumza na waandishi habari juu ya kauli zinazotolewa na baadhi ya watu zenye nia hovu na kuhatarisha usalama wa nchi wakati Dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya Amani tarehe 21 Septemba.
Katika mkutano uliofanyika leo tarehe 17 Septemba 2024 jijini Dar es Salaam,uliojumuisha viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa,Wanawake kutoka makundi maalum ambapo Katibu Mkuu wa chama cha UDP Saum Hussein Rashid amesema “kauli mbalimbali zinazotolewa na baadhi ya vikundi zina dhamira chafu ukilinganisha na mambo makubwa ambayo Rais ameyafanya.
“Kuelekea siku ya Amani tumeona kuna haja ya kusema neno,tunapendekeza kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuamini na kuheshimu uongozi thabiti wa Mwanamke (Rais Samia)
“Tunalaani kwa nguvu zote baadhi ya viongozi wanawake wenye nia hovu ya kudharirisha utu wa mwanamke,kauli hiyo haijatufuraisha na tunaikataa Kwa nguvu zote”
“Rais ambae ni kiongozi mkuu wa nchi ambae majukumu ya ulinzi na usalama anayasimamia yeye kumtuhumu haijakaa sawa.