Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso ameongoza kikao cha wadau wa Sekta ya Maji Mkoa wa Ruvuma wilayani Songea leo tarehe 17 Septemba 2024.
Kikao hicho pia kimeudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Songea na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Damas Ndumbaro na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng.Mwajuma Waziri.
Lengo la kikao hiki ni kuwashirikisha mipango na taarifa ya kazi inayofanyika na inayoendelea kufanyika kwa Sekta ya Maji Wilaya ya Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao hiki; Waziri Aweso amesema amewaelekeza watendaji wa Wizara ya Maji katika mikoa yote nchini vikao hivi kufanyika nchi nzima ili kutoa fursa kwa wadau na viongozi kujua kazi inayoendelea kufanyika chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Maji.
Aidha, Wadau walioshiriki katika kikao hiki wilayani Songea ni Watumishi wote wa sekta ya maji Ruvuma, Mamlaka ya Ya Maji Songea, Waheshimiwa madiwani wote, Mheshimuwa mbunge wa jimbo, wawakilishi wa wabunge, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya kamati ya siasa ya CCM mkoa ikiongozwa na M/Kiti wa CCM Mkoa, kamati ya siasa ya CCM wilaya, wazee wa mila, viongozi wa Dini, Taasisi za Kibenki, wakandarasi wa Miradi ya Maji, makatibu tarafa, na waandishi wa habari.