Halmashauri ya wilaya ya Geita imetangaza rasmi Maeneo ya Kiutawala Majina ya Mipaka ya Vijiji na Vitongoji katika majimbo mawili ya uchaguzi likiwemo Jimbo la Busanda na Jimbo la Geita katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.
Akitangaza Maeneo hayo Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Rajabu Magaro amesema lengo la kufanya vile ni kumfahamisha mwananchi kujua eneo lake la kiutawala sambamba na kutambua viongozi halisi wa Maeneo yake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita , Mh Charles Kazungu amewataka viongozi mbalimbali waliopewa dhamana katika Zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuacha Mzaha kwani Jambo hilo ni la kitaifa na haliitaji kuwekewa mzaha wa aina yoyote.
“Rai yangu kwenu tumeanza tukio hili ni tukio muhimu sana la kitaifa linahitaji weledi na kuacha Mizaha yote kama mlikuwa na mizaha kwa maafisa wenu wa halmashauri sasa hili ni jambo la Kitaifa.” Amesema Mhe Kazungu
Halmashauri ya wilaya ya Geita ina kata 37, Vijiji 145 na Vitongoji 593 ambavyo tayari vimekwisha tangazwa na kugawanywa katika maeneo mbalimbali ya kiutawala.
“Sheria za Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka ya wilaya sura namba 287 kwa Mujibu sura namba 188 zinaelekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa lengo ni kuzifanya serikali za Mitaa ziongozwe kwenye Demokrasia, ” Msimamizi Mkuu Uchaguzi Serikali za Mitaa ngazi ya Halmashauri , Karia Magaro.
“Kwa mujibu wa kifungu cha 101 cha Sheria za Serikali za Mitaa mamlaka ya wilaya sura namba 287 na Kifungu cha 87 cha sheria za Serikali za Mitaa mamlaka za Miji ambayo ni sura namba 288 Waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ana mamlaka ya kutunga kanuni za Uchaguzi za Serikali za Mitaa anapohitajika kuongoza uchaguzi huo, ” Msimamizi Mkuu Uchaguzi Serikali za Mitaa ngazi ya Halmashauri, Karia.