Serikali ya Rwanda imezindua awamu ya majaribio ya kuweka roboti katika mtaala wa kitaifa.
Mpango huu, unaoanza mwaka huu wa masomo, unalenga kuwapa wanafunzi ujuzi zaidi, kuhimiza matumizi ya vitendo ( practical sessions) ya masomo kama vile fizikia, hesabu, Tehama, na kuwahimiza watoto kuwa na fikra za uvumbuzi wa vitu mbalimbali.
Awamu ya majaribio itawashirikisha takriban wanafunzi 3,020.
Walimu 33 kutoka shule 26 kote nchini watakuwa mabalozi wa mpango huo na kuchukua jukumu muhimu katika upanuzi wake.
Mpango huo pia unahusisha watoa huduma watano ambao wanasaidia kubuni zana za elimu zinazowiana na malengo ya kiteknolojia na kielimu ya Rwanda.
Sio wanafunzi wote watasoma moja kwa moja roboti, kwani kozi hiyo itaunganishwa katika masomo yaliyopo.
Wizara ya Elimu nchini humo imesema kuwa mpango huo hautahusisha masomo yanayohusisha sayansi ya kompyuta na fizikia.