Serikali ya Haiti siku ya Jumatano iliunda baraza la muda la uchaguzi lililotafutwa kwa muda mrefu na jumuiya ya kimataifa ili kuandaa nchi hiyo yenye matatizo ya Caribbean kwa uchaguzi wake mkuu wa kwanza tangu 2016.
Smith Augustin, mjumbe wa baraza la mpito la rais nchini humo, alithibitisha kwa The Associated Press kwamba baraza la uchaguzi liliundwa, pamoja na kuwa na wajumbe saba tu kati ya wale ambao kisheria wanastahili kuwa jopo la wanachama tisa. Alisema wanachama wengine wawili huenda wakatangazwa katika siku zijazo.
Baraza la uchaguzi, ambalo linawakilisha makundi ya wakulima, waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu na jumuiya ya Vodou, lina jukumu la kuandaa uchaguzi na kusaidia kuunda mfumo wa kisheria wa kufanya uchaguzi huo.
Haiti haijapata rais tangu Julai 2021, na ilifanya uchaguzi mara ya mwisho mnamo 2016.
Baraza la awali la uchaguzi lilivunjwa mnamo Septemba 2021 na Waziri Mkuu wa zamani Ariel Henry, ambaye alilishutumu kwa “mchama”. Hatua yake ilichelewesha uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 2021 na kuwafanya wakosoaji kumshutumu Henry kwa kushikilia mamlaka, shutuma alizozikataa.