Uanzishwaji wa Mitaala ya ufundishaji kuhusu magonjwa yasiyoambukiza shuleni,upimaji wa magonjwa kwa wanafunzi,kauli nzuri za watoto kwa wazazi na upimaji wa mara kwa mara ni moja ya mikakati iliyoidhinishwa katika kutatua changamoto wanazokumbana nazo wagonjwa hao na jinsi yakuishi uwapo na magonjwa hayo.
Hayo yamebainishwa katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Tanzania Non communicable disease alliance (TANCDA) kuhusu namna ya kutatua changamoto kwa wagonjwa hao leo septemba 19,2024 na Mkurugenzi wa Wizara ya Afya, Kitengo cha Magonjwa yasiyo ambukiza Dk Omary Ubuguyu.
Ameyabainisha hayo ikiwa ni semina ya madaktari,wagonjwa na waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kutatua changamoto kwa wanaoishi na magonjwa hayo na umuhimu wa elimu kuhusu namna ya kumsadia mwathirika wa magonjwa hayo apatapo tatizo.
Aidha, Mabuguyu ameeleza kuwa lengo hasa la semina hiyo ni kusikia sauti ya wanaoishi na magonjwa haya na kujua ni namna gani hasa ya kutatua chamangoto wanazopitia katika huduma za afya na kufanya maboresho katika huduma hizo.
“Moja ya makubaliano tuliyoyafanya leo ni kutengeneza umoja wa wenye magonjwa yasiyo ambukiza ili wawe na kauli ya pamoja lakini pia tumetoa nafasi ya mwakilishi wakutoa ushauri katika huduma zetu tunazozitoa”
Amesema ushauri wao unatupa nguvu sana katika kufanya maamuzi lakini pia wagonjwa hawa wanajukumu la kutoa elimu kwenye jamii ili wanapopata tatizo wapate msaada wa haraka.
Aidha baadhi ya wagonjwa akiwemo Jacquline Adam (40) anaeishi na saratani ya titi iliyoanza mwaka 2016 na kugundulika 2020 anasimulia tatizo hilo lilivyoanza mpaka kugundulika.
“Nilikua na uvimbe ambao baada ya kupimwa niliambiwa kuwa ni uvimbe wa kawaida na kufanyiwa upasuaji ila baada ya miezi 4 ndipo uvimbe ukaanza upya, baada ya vipimo vingine ndipo mwaka 2020 ikagundulika kuwa ni saratani ” amesema
“ Gharama ni nazotumia sizimudu maana ni kubwa na hali hii imeathiri uchumi wangu kwa kupoteza kazi tangu nianze kuugua “ ameeleza
Salim Ali muhitimu wa kidato cha sita anaeishi na tatizo la kisukari anasema kuna umuhimu wa elimu ya magonjwa yasiyoambukizwa kufundishwa mashuleni
“Nilianza kwa kuanguka kwa kuishiwa nguvu bila kujua tatizo ni nini, mpaka siku nilipoishiwa nguvu karibu na wanafunzi wa masomo ya sayansi ila wenzangu wa masomo mengine wa kawaambia huwa wananipatia soda yenye sukari ni napopatwa na tatizo hilo,wenzangu wa sayansi wakagundua ni sukari na ndipo nilipimwa ikawa kweli” amesema
Anaendelea kusisitiza kuwa kuna umuhimu wa elimu ya magonjwa ya siyoambukizwa,mashuleni ni muhimu sana kwakila mwanafunzi kujua dalili na jinsi yakumsaidia mgonjwa wa magonjwa hayo.
Ofisa mradi TANCDA Happy Nchimbi amesema dhumuni kubwa la mradi huu ni kuhakikisha tunatengeneza umoja ili tunapotengeneza sera iweze kutatua changamoto zao zote kwa wakati mmoja.
Aidha Wagonjwa walioshiriki leo ni wagonjwa wa sukari,presha,moyo,seli mundu,saratani na afya ya akili pamoja na chama cha watu wenye kisukari Tanzania
Baadhi ya changamoto wanazopitia wagonjwa hao ni pamoja na gharama kubwa za matibabu hasa unapochelewa kugundua tatizo.