Majeshi ya Israel yamewaua takriban Wapalestina 14 katika shambulio la hivi karibuni la anga na makombora katika maeneo ya kaskazini na kati, kulingana na matabibu.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa maafisa walisema makombora ya Israel yalishambulia kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza, na shambulio la anga likashambulia nyumba moja kaskazini mwa Gaza.
Wakazi pia waliiambia Reuters, kwamba vifaru vilisonga mbele zaidi kaskazini magharibi mwa Rafah – karibu na mpaka na Misri
Jeshi la Israel limesema kuwa vikosi vinavyoendesha shughuli zao mjini Rafah katika wiki zilizopita viliwaua mamia ya wanamgambo wa Hamas, wakapata mahandaki na vilipuzi na kuharibu miundombinu ya kijeshi.
Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takriban Wapalestina 41,270 – ikiwa ni pamoja na watoto 11,355 – wameuawa huko tangu Oktoba 7, na wengine zaidi ya 95,000 kujeruhiwa.