Tamasha la Kitaa Festival la Kampuni ya Coca-Cola limeanza rasmi Jumamosi hii, likiwatembelea wakazi wa Manzese/Bhakresa jijini Dar es Salaam kufurahia utamaduni wa vyakula vya asili vya watanzania.
‘Bakhresa Kitaa Fest’ iliwaunganisha wapishi, mashabiki wa vyakula mbalimbali, watu maarufu, na wapishi mashuhuri kupitia maonesho ya kupika kwa pamoja, wakionesha ubunifu kupitia mapishi hayo.
Wakazi mbalimbali wa maeneo ya Manzese, Mawasiliano Bus Stand, Kimara Mwisho, Malamba Mawili, na Kibamba walishindana kwenye shindano la kuandaa vyakula vya asili, ambapo washindi walipewa zawadi kutokana na ubora wa mapishi yao.
“Tunafurahi sana kuwaletea wakazi wa Manzese/Bakhresa Tamasha la vyakula vya asili la Coca-Cola”.
“Tukio hili la kipekee linaonyesha dhamira yetu ya kuwaunganisha watu kupitia uzoefu wa kupika pamoja kwa vyakula pendwa,” alisema Kabula Nshimo, Meneja Mwandamizi wa Masoko-Coca-Cola Tanzania.
“Hii ni fursa nzuri ya sisi kuungana na wateja wetu, kusherehekea ubunifu wa mapishi, na kuonyesha upekee wa bidhaa ya Coca-Cola kama kinywaji bora kinachoendana na chakula chochote.”
Tamasha hili pia lilijumuisha burudani za muziki kutoka kwa Msanii Mzee wa Bwax, na hivyo kuwafanya wahudhuriaji kufurahia burudani ya muziki kutoka kwa msanii huyo.
Wiki ijayo ni zamu ya wakazi wa Kinondoni ambao nao wanatarajiwa kushuhudia kampeni ya ‘Coca-Cola Food Fest’, ambapo wauzaji wa vyakula maarufu ‘Mama Lishe’ wa maeneo ya Mwinjuma CCM, Msasani, Tegeta Nyuki, Boko, na Goba watashindana vikali kuonyesha ujuzi wao wa kupika. Washindi wa mashindano hayo watasonga mbele kushiriki ‘Kawe Kitaa Fest’ itakayofanyika jumamosi ijayo.
Baada ya Dar es Salaam, kampeni hii ya kusherehekea vyakula vya asili vya kitanzania itafanyika kwenye miji mingine muhimu kama vile Mwanza, Arusha, Mbeya, Morogoro, na Dodoma, pamoja na vyuo vikuu mbalimbali.
Kampeni ya ‘Coca-Cola Food Fest’ sio tu kuhusu chakula—ni jukwaa la ubunifu, likichanganya ladha za vyakula vya asili na kinywaji vya Coca-Cola. Hili ni dhihirisho la ubunifu wa tofauti kutoka Kampuni ya Coca-Cola katika kushiriki kwenye vyakula visivyo sahaulika katika nyakati za pamoja.