Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) limepiga marufuku matumizi ya vifaa vingine vya mawasiliano baada ya mashambulizi mabaya yaliyolenga mshirika wake Hezbollah nchini Lebanon wiki iliyopita, maafisa wa usalama walisema.
Afisa mmoja alisema operesheni kubwa inaendelea na IRGC ili kukagua vifaa vyote, sio vifaa vya mawasiliano pekee.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) limewaamuru wanachama wote kuacha kutumia aina yoyote ya vifaa vya mawasiliano baada ya maelfu ya (redio call) simu za mazungumzo yanayotumiwa na washirika wake wa Hezbollah nchini Lebanon kulipuka katika mashambulizi mabaya wiki iliyopita, maafisa wawili wakuu wa usalama wa Iran waliambia Reuters.
Mmoja wa maafisa wa usalama alisema operesheni kubwa inaendelea na IRGC kukagua vifaa vyote, sio vifaa vya mawasiliano pekee.
Alisema vifaa hivi vingi vilitengenezwa nyumbani au kuagizwa kutoka China na Urusi.
Iran ilikuwa na wasiwasi kuhusu uvamizi wa maajenti wa Israel, wakiwemo Wairani kwenye orodha ya malipo ya Israel na uchunguzi wa kina wa wafanyakazi tayari umeanza, unaolenga wanachama wa ngazi za kati na wa ngazi za juu wa IRGC, aliongeza afisa huyo, ambaye alikataa kutambuliwa kwa sababu ya unyeti wa jambo.