Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Lissu nyumbani kwake Tegeta Jijini Dar es salaam na kuondoka nae.
Taarifa iliyotolewa na ukurasa wa X wa CHADEMA imeeleza yafuatayo “Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Lissu nyumbani kwake Tegeta, msafara wa magari 11 umemchukua na kuondoka nae bila kusema wanampeleka kituo gani cha Polisi”
Tundu Lissu amekamatwa muda mfupi baada ya yeye mwenyewe kuandika kwenye ukurasa wake wa X akisema “Gari tatu za Polisi zikiwa na Maafisa wa Polisi zipo nje ya nyumba yangu, wamenijulisha natakiwa kupelekwa kwa RCO Kinondoni, najiandaa kwenda”