Staa na mwanamuziki na mwandishi Usher Raymond anasema kwamba akaunti yake ya X (zamani ya Twitter) ilidukuliwa baada ya mashabiki kugundua anafuta post zake alizowahi kuwa na rapper Pdiddy.
Watumiaji kwenye jukwaa hapo awali walitoa nadharia kwamba mwimbaji huyo mashuhuri alikuwa akifuta machapisho yake katika juhudi za kuficha uhusiano wake na Diddy baada ya mogul huyo wa Bad Boy kukamatwa, wiki iliyopita.
Usher alifafanua hali hiyo katika chapisho la Jumapili usiku. “Akaunti ilidukuliwa sipo nayo! [Emojis za kucheka] Tutaonana usiku wa leo Intuit Dome,” aliandika.
Mashabiki kwenye majibu hawakuwa wote wananunua uongo wa maelezo yake na hawakusita kucomment.
“Hakuna mtu anayeamini uongo wako Afadhali ujipatie kisiwa kizuri ili kwenda na kukaa huko kwa muda,” mtumiaji mmoja aliandika.
Mwingine aliandika: “Ni wazimu sana jinsi eti account ilivyodukuliwa…lakini badala ya kuchapisha mambo ya tofauti, mdukuzi AMEFUTA machapisho yako na Diddy ?ndio amekamatwa…na mambo yote na Justin Bieber tumeyaona. Cha ajabu sana unakana’ Sawa kaka.”
Mamlaka ilimkamata Diddy Jumatatu iliyopita na alikanusha mashtaka ya ulanguzi wa ngono na ulaghai siku iliyofuata.
Wakili wake, Marc Agnifilo, hakuweza kumtoa kwa dhamana na kwa upande wake, anasubiri kesi yake katika Kituo cha Kizuizi cha Metropolitan huko Brooklyn.