Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma leo Septemba 23, 2024 limefanya doria za magari na miguu katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa ajili ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kupita mitaani na silaha mbalimbali.
Doria hizo zilizokua na Askari pamoja na mbwa wakali zimeongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Filemon Makungu huku akisema polisi kuzagaa mitaa mbalimbali kwa Kigoma hakusiani na swala la maandamano bali ni zoezi la kawaida ambalo litabaki kua endelevu na wananchi wasipate taharuki yoyote.
“Tulikua na doria ya kawaida kuimalisha ulinzi na hali ni swali na kwa kigoma watu wanatii sheria bila shuruti na doria hii haihusiani na swala la maandamano na kigoma hakuna maandamano hii ni doria ya kwetu tu ya kawaida na ni endelevu na kigoma hatujapata taarifa za watu kuandamana”-RPC Kigoma
ikumbukwe Septemba 11, 2024 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na mauaji, yakiwemo ya makada wake, Ali Kibao. Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku ambapo siku ya leo katika mikoa mbalimbali polisi wameonekana sana wakilinda na kupita na magari yao kama sehemu ya kutazama hali ya ulinzi na usalama.