Wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi, waandishi wa habari wana wajibu wa kuhamasisha ushiriki wenye kuheshimu amani, uchaguzi huru na wa haki.
Katika uchaguzi mkuu vyama vya siasa vya nchini vinatumia mitandao ya kijamii kufikisha taarifa na mbalimbali hivyo kampeni nyingi huenda zikachukua sura ya tofauti.
Matumizi ya mtandao sasa yanakuwa kwa kasi na kusaidia wengi kupata au kueneza taarifa mbalimbali ,lakini mitandao hii wakati wa uchaguzi pia husaidia vyanzo mbalimbali vya habari kukusanya taarifa na kusambaza taarifa kwa umma kwa kuzingatia sheria na miongozo ya habari pasina kuvunja sheria.
Katika kuelekea uchaguzi umuhimu wa intaneti ni mkubwa sana ukizingatia kuwa vyombo vya habari na mitandao kama faceboo,Instagram,X na mengineyo hufuatliwa zaidi kwani wao husambaza taarifa kirahisi na kwa haraka kwa wananchi.
Mashirika mbalimbali sasa yanaangazia ni kwa namna gani itakavyokuwa juu ya matumizi ya intaneti kwenye chaguzi ili kuondoa hali ya sintofahamu iliyopo hasa kwa waandishi wa habari nyakati za uchaguzi kwani hali ya kuzimwa kwa mtandao zinawanyima uhuru wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Ni muhimu wanahabari kuelimisha jamii juu ya mchakato wa uchaguzi, wapate uelewa wa utofauti ya uchaguzi na ilani za vyama, lakini pia watambue umuhimu wa kujitokeza kupiga kura na thamani ya kura zao katika kuleta mabadiliko,hivyo ukosefu wa mtandao huenda usitoe mwanya wa taariza za usahihi kwa wakati sahihi nchini
Kuzimwa kwa Mtandao ni “kukatizwa kimakusudi kwa mtandao na mawasiliano ya kielektroniki, na kuzifanya zisifikike au zisitumike kwa urahisi, kwa eneo mahususi au ndani ya eneo mara nyingi ili kudhibiti mtiririko wa habari.