Vita vya Israel dhidi ya Gaza vimeingia siku yake ya 355, na hadi sasa vimesababisha vifo vya Wapalestina wasiopungua 41,467 na kujeruhi wengine zaidi ya 95,921.
Aidha, inaripotiwa ni zaidi ya watu 10,000 wanahofiwa kufukiwa chini ya vifusi vya nyumba zilizoshambuliwa, Mapigano hayo yalianza tarehe 7 Oktoba, baada ya kundi la Hamas kufanya shambulizi kubwa ndani ya Israel, lililosababisha vifo vya watu 1,200.
Tangu shambulizi hilo, takwimu zilizotolewa na mamlaka za Ukanda wa Gaza zinaonyesha kuwa idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kutokana na mashambulizi makali ya vikosi vya Israel kwa njia ya ardhi na angani.
Lengo la Israel katika operesheni hii ni kuondoa kabisa kundi la Hamas, ambalo limetajwa kuwa la kigaidi na Israel pamoja na Marekani, Umoja wa Ulaya, na mataifa mengine ya Magharibi.
Vita hivyo vimeacha athari kubwa kwa raia, huku maelfu wakijeruhiwa au kupoteza maisha na familia nyingi zikikosa makazi, Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikihimiza pande zote kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kupata suluhu ya kudumu katika eneo hilo.