Nchi kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na mataifa mashuhuri ya Kiarabu, zile za G7 na Umoja wa Ulaya, zinataka kusitishwa kwa uhasama kati ya Israel na Hezbollah kwenye mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Alhamisi.
Alipoulizwa kuhusu kukataa kwa Israel pendekezo la kusitisha mapigano Lebanon inayoungwa mkono na Marekani, Blinken aliiambia MSNBC: “Ulimwengu unazungumza kwa uwazi kwa karibu nchi zote muhimu za Ulaya na katika eneo hilo juu ya hitaji la kusitisha mapigano.”
Aliongeza kuwa atakutana na maafisa wa Israel mjini New York baadaye siku ya Alhamisi.