Kampuni ya Sun King imefungua maduka matatu ya kisasa ya vifaa na mtambo mpya wenye uwezo mkubwa wa kuwezesha matumizi ya umeme jua katika juhudi za kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania za nishati safi , salama na kutuza mazingira hapa nchini.
Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa maduka hayo ya kisasa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo, Msanii Mrisho Mpoto, alisema kwamba vifaa na mitambo ya kampuni hiyo ni mbadala mkubwa wa majenereta ambayo kwa kiasi kikubwa yanaleta moshi na makelele kwenye miji na kuchafua mazingira.
“Hizi ni jitihada za kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika nishati safi na salama na siku ya leo tunasherekea mpango huu unaolenga kubadilisha maisha. Kama wengi wenu mvyojua, upatikanaji wa nishati safi na salama ni msingi wa maendeleo, elimu, afya, pamoja na kuchangia ubora wa maisha kwa ujumla,”alisema.
Alisisitiza kwamba kampuni hiyo imeamua kufungua maduka hayo maeneo ya Temeke, Buguruni na Mwenge katika harakati za kuwaletea karibu wakazi wa jijini Dar es Salaam huduma za Sun king katika maeneo yao na kurahisisha biashara zao za kila siku na shughuli zao za nyumbani yakiongeea mtandao wa maduka yake mkoani Dar es Salaam yaliyopo maeneo mbalimbali ikiwemo Bunju, Kigamboni, Gongo la Mboto, Mbagala, Chanika
“kifaa hiki cha kisasa cha kubadilisha mkondo wa umeme kinaweza kuwasha jokofu , komputa mpakato, taa , waya za ulinzi za umeme na vifaa matumizi vingine kwa gharama na nafuu na mteja anaweza kununua kwa njia ya mkopo na kulipa kidogo kidogo,” aliongeza msanii huyo Mpoto ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Bw. Mpoto alisema kwamba hivi karibuni kule Arusha kampuni hiyo ilifunguka mtambo wa kisasa kwenye hospitali ya jijni humo ili kusaidia wakinamama wakati wa kujifungua pindi umeme unapokatika na kupunguza atha ya mgao wa umeme.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Albert Msengezi alisema kwamba kampuni hiyo kwa sasa imesambaa nchini nzima na wanazidi kwenda vijini katika juhudi za kuwaletea watanzania mapinduzi ya umeme jua kwa kutumia nishati safi na kutunza mazingira.
“Leo tumezindua maduka yetu matatu hapa Dar es Salaam lakini tuna mengine maeneo ya chanika , vikindu na sehemu za pwani katika juhudi za kuleta suluhishi za nishati ya jua zinazopatikana kwa bei nafuu na kuchochea biashara endelevu na uchumi wa nchini, alisema Bw Msengezi
Pamoja na mambo mengine , Bw Msengezi alisema kwamba kifaa hiki kipya kinapanua huduma za Sun king kwenye mkondo wa waya za umeme jua na ikikamilisha na safu ya nguvu ya kituo cha umeme jua yenye nguvu nyingi kuongeza waya ambayo upo kwenye mkondo wa kifaa cha kubadilisha mkondo wa umeme za Sun King.
“ikikamilisha safu ya kifaa cha kisasa chenye nguvu , ambayo ina uwezo wa kutoa kutoka 3.3 kVA hadi 20 kVA AC. Kifaa hiki kimeundwa kwa mahitaji makubwa zaidi, kutoka nyumbani na biashara hadi shule na vituo vya afya, ikitoa uhuru kamili wa nishati na suluhisho zinazoweza kubadilishwa,” alifafanua.
Aliongeza kwamba maduka haya mapya ni viashiria vya hatua muhimu katika dhamira ya kampuni hiyo ya kuwawezesha wananchi na jamii kupitia suluhisho za nishati endelevu huku ukionyesha ubunifu mpya wa kampuni katika teknolojia ya jua.
Kwa upande wake Bw Seth Mathemu, Meneja Mwandamizi Masoko alisema kwamba uzinduzi wa kifaa hicho (Solar Energy Inverter) ilikuwa ni ahadi ya kampuni hiyo kutoa suluhisho za nishati zinazoweza kuaminika na za bei nafuu kwenye ngazi ya familia na biashara kwa watanzania.