Iran kupitia Wizara yake ya mambo ya kigeni inasema haitawatuma wanajeshi wake nchini Lebanon au katika Ukanda wa Gaza kupigana dhidi ya wanajeshi wa Israeli.
Taarifa ya Iran inakuja wakati huu Israeli ikiripotiwa kuendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya ngome za washirika wa Tehran mashariki ya kati.
Israel katika siku za hivi karibuni imekuwa ikitekeleza mashambulio mazito ya angani nchini Lebanon kuwakabili wapiganaji wenye silaha inayosema wanaungwa mkono na Iran katika eneo la mashariki ya kati ikiwemo Syria, Yemen na Iraq.
Tangazo hili linakuja baada ya shambulio la Israeli la Ijumaa ya wiki iliopita kumuua kiongozi wa wapiganaji Hezbollah Hassan Nasrallah.
Nasrallah aliuawa wiki iliyopita katika shambulio la anga la Israel kwenye kituo cha makomando wa kusini cha Hezbollah, ambacho kinatajwa kuwa ni shirika la kigaidi na Marekani, huku Umoja wa Ulaya ukiorodhesha mrengo wake wenye silaha lakini si chama chake cha kisiasa