Rapa 50 Cent hivi sasa ametengeneza vichwa vya habari baada ya utabiri mkali juu ya utajiri wake hii ni baada ya hivi majuzi, kuonyesha dola milioni 3.5 kwa pesa taslimu wakati alipo piga picha na kuonesha umma na sasa anadai kutaka kuwa rapa Bilionea nchini Marekani.
Katika kipindi cha The Enthusiast Podcast, 50 Cent alimwambia Lincoln Salazar, “Nitavunja rekodi nambari hiyo … katika miaka mitano ijayo, amini hilo.” Anaweka ratiba ya uhakika juu ya matarajio yake yakua bilionea.
Zaidi ya kufikia hadhi ya bilionea, 50 Cent alieleza kuwa mtazamo wake utahamia kuwasaidia wengine.
Alisema, “Tayari nina kila kitu ninachotaka … kazi ni: ni kiasi gani unasaidia watu.”
50 Cent anatazamia kwa ujasiri hadhi ya Ubilionea huku akifuatilia kwa makini masuala ya kijamii.