Nchini Rwanda, watu watano zaidi wameripotiwa kufariki kutokana na maambukizo hatari ya virusi vya Marburg na kufikisha idadi kamili ya waliofariki kuwa 11 kwa mujibu wa Wizara ya afya kwenye taifa hilo.
Watu 29 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo tangu mwazoni mwa tarehe 27 ya mwezi Septemba wakati kisa cha kwanza kiliporipotiwa.
Kwa mujibu wa Wizara ya afya katika taifa hilo la Afrika Mashariki, wagonjwa 19 wametengwa na wanapokea matibabu katika hospitali mbalimbali.
Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika CDC kimeripoti kwamba idadi kubwa ya watu walioambukizwa ni wahudumu wa afya ambapo watu wengine zaidi ya 290 waliotangusana na watu walioambukizwa wamepatikana.
Marburg imetajwa kuhusishwa na maambukizo hatari ya Ebola ambayo yamesababisha madhara makubwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi.
Virusi hivyo vinaripotiwa kuambukizwa kutokana kwa mgonjwa hadi mwengine kupitia chembe chembe iwapo watagusana.