Karibia watu 25 wanaohifiwa kufariki baada basi la shule ambalo lilikuwa likiwasafirisha wanafunzi 44 pamoja na walimu wao kuteketea nchini Thailand.
Waziri Mkuu Paetongtarn Shinawatra amethibitisha kutokea kwa vifo kwenye mkasa huo na kutoa pole kwa familia za walioathirika.
Naye Waziri wa masuala ya uchukuzi Suriya Jungrungreangkit ameeleza kwamba idadi kamili ya watu waliofariki katika ajali hiyo haijulikani japokuwa hatima ya watu 25 haikuwa imejulikana.
Jungrungreangkit amewaambia waandishi wa habari kwamba watu 44-walikuwa wameabiri basi hilo, ambapo wanafunzi walikuwa 38 na walimu wanane.
Takriban watu 20,000 wanauawa kila mwaka kwenye barabara za Thailand — wastani wa zaidi ya 50 kwa siku.
Hii ina maana kwamba Thailand ina barabara ya pili kwa vifo zaidi barani Asia baada ya Nepal, na inashika nafasi ya 16 duniani kwa vifo vya trafiki, pamoja na Chad na Guinea-Bissau, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kulikuwa na vifo 25.7 kutokana na majeraha ya trafiki kwa kila watu 100,000 mnamo 2021 nchini Thailand, ikilinganishwa na wastani wa kimataifa wa 15.
Shirika la usalama barabarani la Thai RSC linasema kuwa tayari mwaka huu kumekuwa na vifo zaidi ya 10,000 na majeruhi 600,000 katika barabara za nchi hiyo.
Zaidi ya vifo vinne kati ya vitano vinahusisha pikipiki, RSC inasema, ikilinganishwa na wastani wa kimataifa wa mtu mmoja kati ya watano.