Papa Francis atoa wito kwa siku ya maombi ya amani mnamo Oktoba 7, siku ya kumbukumbu ya shambulio baya la Hamas dhidi ya Israeli, huku hali ya wasiwasi Mashariki ya Kati ikiongezeka.
Katika kipindi chote cha upapa wake wa miaka 11, Francis ameita siku za kufunga na kuomba kwa ajili ya migogoro mingine, kutoka Syria hadi Ukraine.
“Tarehe 7 Oktoba, ninaomba kila mtu aishi siku ya maombi na kufunga kwa ajili ya amani duniani,” papa huyo mwenye umri wa miaka 87 anasema baada ya misa katika uwanja wa St Peter’s.
“Kuna haja ya hili, hasa katika saa hii ya kushangaza ya historia yetu, wakati pepo za vita na moto wa vurugu unaendelea kuvuruga watu na mataifa yote,” anaongeza.
Papa, ambaye atazuru Kanisa kuu la Roma la Santa Maria Maggiore siku ya Jumapili kuombea amani, ametoa wito mara kwa mara wa kukomeshwa kwa migogoro katika Mashariki ya Kati.