Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kupitia Idara ya Sanaa ya Ubunifu, kimeandaa shindano la sanaa lililopewa jina la Uzuri wa Tanzania Fahari Yangu, linalolenga kukuza Ubunifu kwa vijana wa Kitanzania kuanzia wanafunzi wa sekondari kidato cha kwanza hadi cha sita Tanzania nzima na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dr, Erick Mgema, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema shindano hilo linasherekea Ubora wa kisanii lakini likilenga kuhimiza Utalii wa ndani hapa nchini.
Naye Dr, Issa Mbura ambaye ni mhadhiri kutoka idara ya Sanaa ya Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema washiriki wanapaswa kuchora picha zitakazoakisi uzuri wa Tanzania.
” Washiriki watanufaika na semina ya mafunzo ya siku mbili katika chuo cha wachoraji ikifuatiwa na vikao vya uchoraji vya siku 8, lakini pia washiriki watakaoingia fainali michoro ya itahukumiwa na kuonyeshwa wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi itakayofanyika mapema Novemba mwaka huu katika Chuoni”. Amesema Dkt Mbura.
Hata hivyo Aileen Meena kutoka Vivo Energy Tanzania, amesema ” Shindano hilo la sanaa linalenga kuwawezesha wasanii vijana na dhamira yetu kuonyesha ubunifu na uwajibikaji wa kijamii kwa kutoa jukwaa kwa vijana kusherekea uzuri wa Tanzania “, amesema Meena.