Waziri wa zamani wa Baraza la Mawaziri wa Singapore alihukumiwa Alhamisi kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukiri mashtaka ya kupokea zawadi haramu, katika kesi ya nadra ya jinai inayomhusisha waziri katika kituo cha kifedha cha Asia.
Aliyekuwa waziri wa uchukuzi Iswaran alikiri juma lililopita shtaka moja la kuzuia haki na manne ya kupokea zawadi kutoka kwa watu ambao alikuwa na biashara nao rasmi alikuwa waziri wa kwanza kushtakiwa na kufungwa
Jaji Vincent Hoong, katika uamuzi wake, alisema wenye vyeo vya juu “lazima watarajiwe kuepuka dhana yoyote kwamba wanaweza kuathiriwa na faida za kifedha”.
Upande wa utetezi ulikuwa umeomba kifungo kisichozidi wiki nane, huku upande wa mashtaka ukisisitiza kifungo cha miezi sita hadi saba.
Mahakama iliidhinisha ombi la Iswaran kuchelewesha kuanza kwa kifungo chake hadi Jumatatu, Channel News Asia iliripoti.
Anaendelea kuwa nje kwa dhamana kwa sasa. Haijabainika iwapo atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Awali Iswaran alishtakiwa kwa makosa 35, lakini waendesha mashtaka waliendelea na makosa matano tu, huku wakipunguza mashitaka mawili ya rushwa hadi kupokea zawadi zisizo halali.
Iswaran alipokea zawadi zenye thamani ya zaidi ya dola 74,000 za Singapore (£43,290) kutoka kwa Ong Beng Seng, tajiri mkubwa wa mali wa Malaysia mwenye makazi yake Singapore, na mfanyabiashara Lum Kok Seng.