Idadi ya vifo vya kimbunga Helene nchini Marekani ilifikia 200 baada ya majimbo ya Georgia na North Carolina kuripoti vifo zaidi.
Idadi iliyosasishwa ya vifo, maradufu ya ile ambayo maafisa walikuwa wameripoti hapo awali, inakuja wakati Rais Joe Biden alitembelea maeneo yaliyoharibiwa na dhoruba huko Florida na Makamu wa Rais Kamala Harris alifanya safari tofauti kwenda Georgia mnamo Alhamisi.
Kimbunga cha Helene, kimbunga cha aina ya 4, kilisababisha mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa, na kusomba nyumba na magari na kuwadai wahasiriwa kote kusini mashariki mwa Amerika.
Mamia ya watu bado hawajulikani walipo na zaidi ya milioni moja wamesalia bila umeme wiki moja baada ya kimbunga hicho kutua Septemba 26. Operesheni kubwa ya kutafuta na kuokoa bado inaendelea.