TAMASHA la Miaka 60 ya Msondo Ngoma Music Band Baba ya muziki linatarajia kufanyika Oktoba 26 mwaka huu katika viwanja vya Gwambina Lounge zamani TCC Club Changombe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Kibiriti, amesema kuwa bendi hiyo itaweka kambi ya wiki mbili mkoani Dodoma kwa nia ya kujifua zaidi.
“Msondo ngoma tuna jambo letu la Miaka 60 kuanzishwa tamasha la sasa litakuwa na vitu vizuri na ubunifu ndani ya miaka 10 iliyopita baada ya kuadhimisha miaka 60 wamejiunga wanamuziki wengi.”
“Miaka 60 ya Msondo Ngoma Bendi itaanza na kisomo kitakachofanyika Oktoba 13 Amana ofisini za bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka waimbaji waliotangulia mbele za haki.
“Waimbaji wanafanya mazoezi ya kutosha siku hiyo wataimba ‘live’ ili kukonga nyoyo za mashabiki zao wanaoipenda Msondo Ngoma wakati wote wanapotoa burudani.”amesema Kibiriti
Aidha Kibiriti amesema , Band zitakazosindikiza siku hiyo ni Twanga Pepeta chini ya Chaz Baba, Bogoss Musica Chini ya Nyoshi Elsaadat na Spidoch Band ‘ Wazungu Weusi’ chini ya Pasia Budas
Wasanii wengine Freshi Jumbe, anayeishi nchini Japan aliyetamba na wimbo wa ‘penzi ni kikoozi, Ally Choki na Mwanamuziki wa bongo fleva Ben Pol.
Fresh Jumbe amesema, miongoni mwa waimbaji wa bendi ya Msondo ameimba nao nyimbo nyingi na zingine atazifanyia mazoezi na ataimba siku hiyo.
Ally Choki amesema kuwa siku hiyo ataimba wimbo alioimba na Mzee Ngurumo Baba ulichomtendea Mama pamoja na husia wa wazazi.
Naye Juma Katundu maarufu kama ‘JK’ amesema kuwa ni kitu kikubwa kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano siku hiyo
Hata hivyo Pasia Budas kutoka Spidoch band amesema, kutokana na umri aliokuwa nao, amefurahi kupata nafasi ya kuwasindikiza bendi hiyo kwenye miaka 60 yao na amehaidi kutoa burudani nzuri na kuimba live wimbo wa kilio cha mtu mzima.
Tamasha la miaka 60 kiingilio ni Laki moja, Elfu 50 na kawaida 15000 ukichukua tiketi yako mapema, siku ya Tamasha mlangoni kiingilio ni Elfu 20 mlangoni.