Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon na kuongeza msaada wa kimataifa wa kibinadamu wakati wa ziara yake katika mji mkuu Beirut.
Baada ya kukutana na familia zilizokimbia mashuleni, Filippo Grandi alisema “wanachohitaji zaidi ni mashambulio ya anga kukoma ili waweze kurejea nyumbani salama. Usitishaji vita nchini Lebanon unahitajika sana”.
Grandi pia alikutana na Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati, kujadili msaada kwa wale walioathiriwa na mzozo. Kamishna alisisitiza kiwango kikubwa cha mahitaji na hitaji la dharura la msaada zaidi.