Mashambulizi ya mwaka mzima ya Israel dhidi ya Gaza yamesababisha hasara kubwa ya binadamu na mali.
Kwa mujibu wa data iliyotolewa Septemba 30 na ofisi ya vyombo vya habari ya Gaza, jeshi la Israel limefanya karibu mauaji 3,650 katika mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 41,800 wameuawa na zaidi ya 96,800 kujeruhiwa, huku watu 10,000 bado hawajulikani walipo au inadhaniwa wamekufa chini ya vifusi.
Miili ya Wapalestina 520 iliopolewa kutoka kwa makaburi saba ya halaiki iliyopatikana hospitalini.
Watoto ni asilimia 42 ya waliofariki, wanawake 27% na wanaume 31%.
Watoto wamebeba mzigo mkubwa wa mashambulizi ya Israel, huku watoto wachanga 171 wakifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa na watoto wachanga 710 chini ya mwaka mmoja kuuawa. Hata vijusi vimepatikana chini ya vifusi. Takriban watoto 25,973 walipoteza mzazi mmoja au wote wawili.