Hatma ya dhamana kwa Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob anayekabiliwa na kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni inatarajiwa kujulikana leo October 7, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi.
Jacob ambaye ameshinda Uenyekiti wa Kanda ya Pwani kupitia chama chake cha CHADEMA huku akiwa mahabusu tangu September 19,2024 baada ya kuwekewa mapingamizi ya dhamana kutoka Upande wa Serikali licha ya kwamba kesi yake inadhaminika.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga ambapo awali alitupilia mbali maombi ya Serikali juu kiapo cha ziada katika kiapo cha awall.