Rwanda imeanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Marburg tangu Jumapili Oktoba 6, 2024, gonjwa ambao umesababisha vifo vya watu 12 kati ya wagonjwa 41 walioorodheshwa nchini humo tangu mwisho wa mwezi uliopita.
Dozi 700 zinazotumwa na taasisi ya utafiti ya Marekani zimekusudiwa watu walio hatarini zaidi na ambao bado wako katika awamu ya majaribio.
Siku ya Jumamosi Rwanda ilipokea, kutokana na usaidizi wa kifedha kutoka kwa utawala wa Marekani, dozi 700 kutoka kwa Taasisi ya Marekani ya Sabin Institute, chanjo ambayo bado iko katika majaribio ya awamu ya 2 nchini Uganda na Kenya.
Lakini pia tiba za majaribio kutoka kwa maabara ya Californian Mapp.
Hakuna chanjo yoyote kati ya nne au matibabu yanayotathminiwa na Shirika la Afya Duniani ambayo bado yameidhinishwa au kupasishwa kwa majaribio nje ya maeneo ya mlipuko.