Takwimu cha Kituo cha kudhibiti Magonjwa NCDC kimeonesha kuwa hilo ni ongezeko la asilimia 239 katika kipindi kama hiki mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 350 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Nigeria katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu wa 2023.
Mamlaka nchini Nigeria zinasema ugonjwa huo sio kawaida nchini humo lakini kwa sasa maeneo mengi nchini huyo yanakabiliwa na ukosefu wa maji safi na salama na makazi duni mijini na vijijini.
Idadi ya washukiwa wa ugonjwa wa kipindupindu iliongezeka kutoka 10,837,hadi kutoka 3,387 mwaka uliopita, na wengi wa wale walioathirika kuwa ni watoto chini ya miaka mitano.
Nigeria inakabiliwa na janga hilo wakati ambapo inakabiliwa na mafuriko ambayo yamesababisha takriban watu milioni 2 kuyahama makazi yao.