Kesi inayomkabili Afisa wa Jeshi la Polisi ‘AFANDE’ Fatma Kigondo ya kuratibu kubaka na kulawiti kwa kundi kwa Binti wa Yombo Dovya, Jijini Dar es salaam imeahirishwa leo Oktoba 07, 2024 katika Kituo jumuishi cha Utoaji haki Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Dodoma ambapo ilipangwa kusikilizwa.
Kutokana na kushindwa kufika kwa Mtuhumiwa ambaye imeelezwa ni mgonjwa, hivyo Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2024.
Baada ya Kesi hiyo kuahirishwa Wakili wa upande wa mlalamikiwa Cedric Mbunda amezungumza na Wanahabari nje ya kituo hicho na kusema kuwa wameiomba Mahakama kuahirisha Kesi hiyo kutokana na kwamba mteja wake hayupo vizuri kiafya hali iliyopelekea mabishano ndani ya Mahakama huku Upande wa mlalamikaji ukitaka Afande huyo kufika hata kama ni mgonjwa.