Mahakama ya Juu ya Brazil iliidhinisha mtandao wa X zamani Twitter kurejea tena na huduma nchini humo siku ya Jumanne, baada ya mtandao huo wa kijamii kubadili namna ya uendeshaji wake na kuanza kutii maamuzi ya mahakama ambayo mmiliki wake bilionea Elon Musk alikuwa ameapa kukataa.
Jaji wa Mahakama ya Juu Alexandre de Moraes, ambaye alikuwa amezuiliwa kwa muda wa miezi mtandao wa Musk, alimpa mwanga wa kijani kuanzisha tena shughuli katika nchi hiyo kubwa zaidi ya Amerika ya Kusini kuanzia mara moja.
Katika uamuzi huo, Moraes alisema X alikuwa amekidhi mahitaji yote muhimu ili kuanza kufanya kazi tena nchini.
Musk, ambaye alikuwa ameshutumu amri hizo kama udhibiti na kumwita Moraes “dikteta,” alianza kubadili msimamo wake katika wiki za hivi karibuni, na mtandao wake wa kijamii kuzuia akaunti zilizoripotiwa na mahakama.
Moraes, katika uamuzi wake wa Jumanne, aliamua kuwa kampuni ya mawasiliano ya Brazil Anatel lazima ifanye haraka ili kuruhusu X kurejea ndani ya saa 24.