Katibu wa Baraza la Sanaa Zanzibar BASSFU Juma Chum amesema midoli inayoekwa kwenye maduka Zanzibar inaweza kupelekea vishawishi vibaya kutokana na Midoli hiyo kua na taswira pindi inapovalishwa nguo zisizofaa ambazo serikali imekua ikakataza na kupiga marufuku midoli hiyo ambayo inadaiwa kukiuka mila na Desturi za Zanzibar
Chum akizungumza na Ayo tv maara Baada ya Msako wa Siku Tatu visiwani Zanzibar wa kutokomeza midoli hiyo inayotajwa kua inavunja maadili pindi watoto na wakaazi wa Zanzibar kuitazama midoli hiyo amesema wafanyabiashara wa Zanzibar Kosa wanalofanya ambalo Baraza hilo limepiga marufuku ni kueka Midoli nje ya maduka na kuvesha nguo zinazokiuka Mila na Silka ya Zanzibar
” Ule Mdoli una taswira flani kwa sababu ule mdoli una taswira flani ambayo imejengaka baada ya muonekana wa nguo hiyo inayouzwa sasa inaweza kuleta vishawishi vibaya ,sisi kama serikali kwa umoja wetu idara mbali mbali ,Mashirika mbali mbali tunakemea vitendo vya udhalilishaji, Sasa ile midoli wakati mwingine inaibua hisia —Katibu Baraza la Sanaa Zanzibar Juma Chum “