Jiji la Arusha limeanza zoezi la watu kujiandikisha na kujitokeza kwa kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya kupata haki ya msingi ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake,Msimamizi wa uchaguzi,John Kayombo amesema kuwa ,maandalizi yote yamekamilika na hadi kufikia oktoba 20 mwaka huu katika vituo vyote 462 ,kuanzia saa 2 hadi saa 12 jioni.
Ameongeza kuwa,mpaka sasa kuna jumla ya vituo 462 vya kujiandikishia ambavyo vitasaidia sana wananchi kutokaa kwenye foleni kwa muda mrefu na kuondoa msongamano .
“Tuna vituo 462 tumeamua kuboresha kwa kuongeza vituo ili kusudi kutowafanya watu wasimame kwa muda mrefu kwenye vituo vya kujiandikisha na tutafanya hivyo na wakati wa kupiga kura ,tunaomba watu wote wajitokeze ,mtu ambaye hatajiandikisha ,hata pata fursa ya kupiga kura”
Ameeleza kuwa, tangazo la serikali namba 574 la mwaka 2024 nakala za viapo zimetolewa kwa viongozi wa vyama ili kuwarahisishia mchakato wa kuapisha mawakala .
Alifafanua kuwa ,orodha ya vituo vyote vya kujiandikisha kwa vyama vya siasa na.upangaji wa vituo umezingatia azma ya kupunguza foleni ili kuruhusu watu kujiandikisha kwa wepesi na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji Mali.
Kayombo ambaye pia ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha amewataka wananchi kutambua kuwa uchaguzi huu ni muhimu sana kwani wanakwenda kuchagua viongozi watakaoshughulika na mambo ya wananchi na maisha yao ya kila siku