Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes amedai kuwa hana shaka kuhusu ubora wa kocha wa Sporting CP Ruben Amorim.
Amorim anahusishwa na kibarua cha Pep Guardiola katika Manchester City huku kukiwa na mazungumzo ya mkuu wa soka wa Sporting Hugo Viana kuhamia Uingereza kuchukua nafasi ya Txiki Begiristain anayeondoka.
Fernandes alisema: “Michezo si kitu kipya, tangu Amorim awasili imekuwa timu bora yenye soka bora, thabiti na yenye usajili sahihi.
“Wamekuwa mabingwa na wanaanza mwaka huu tayari mbele, wamejiandaa vya kutosha na kuhusu Amorim nimezungumza mara nyingi.
“Ni kocha anaonyesha amejipanga kwa sababu kutwaa ubingwa pale Sporting si jambo jepesi, kwa miaka 20 walikuwa hawajashinda na tayari wameshinda miwili, iwapo anaweza kufanya hivyo huko England au kwingine haitajulikana hadi anafika huko, lakini ubora uko machoni pa kila mtu.”