Siku ya leo umefanyika mkutano wa waandishi wa Habari juu ya tamasha la Samia Fashion Festival linatarajiwa kuzinduliwa, likiwaunganisha pamoja vipaji vikubwa vya mavazi vya Tanzania, wataalamu wa sekta hiyo, na wahusika wa kitamaduni likiandakiwa na wadau wa fashion nchini wakiongozwa na Khadija Mwanamboka akiwemo Martin Kadinda
Tamasha hili limepewa jina kwa heshima ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na limelenga
kukuza utamaduni wa Tanzania kupitia mavazi huku likionyesha mchango wa Rais katika sekta ya ubunifu.
Tamasha litaendelea kwa siku saba, likijumuisha matukio mbalimbali ya kuwawezesha wanawake, watoto, na vijana kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Kauli mbiu ya tamasha hili ni “Ubunifu na Stara”. kauli mbiu hii ni taswira tosha ya nafasi nahaiba ya mama yetu mpendwa Dkt Samia Suluhu Hassan, na kwa. Jinsi gani jamii inaweza
kutumia haiba hiyo yenye stara katika nyanja mbali mbali za kijamii, kama vile motiko, sherehe, shughuli za jioni, malezi, na kadhalika.
Tamasha hili ni fursa kwa wabunifu kutuma kazi zao, ambazo zitapitiwa na jopo la majaji wetu mahiri na wazoefu katika sekta ya mitindo wakiongozwa na Chief Judge Mwanamitindo Miriam Odemba, Mwanamktindo wa Kitanzania anayeishi Ufaransa..
Mwanzishilishi Wa Tamasha hili Khadija Mwanamboka amesema “Tamasha hili si sherehe ya mavazi tu; ni jukwaa la kuonyesha ubunifu wa Kitanzania na ni heshima kwa uongozi na maono ya Mama Samia Suluhu Hassan,”
#MillardayoUPDATES