Zaidi ya wananchi elfu Mbili wa Mji wa Ifakara Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro wamefanya matembezi ya pole zaidi ya kilometa 5 Ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura katika Mji huo.
Matembezi hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya ambapo amewataka wananchi kuendelea kujitokeza katika zoezi hilo ambalo limeanza tangu octoba 11 hadi octoba 20 mwaka huu.
DC Kyobya amesema zoezi hilo la kujiandikisha ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu nchini.
Ameongeza Kwa kusema kuwa Kila mwananchi ambaye anasifa ya kupiga kura anahaki ya kujiandikisha na hakuna mtu yoyote ambaye anaweza kumzuia.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ifakara Mji Bi. Zahara Michuzi amesema hamasa imefanyika Kwa kiwango kikubwa na wananchi wanaendelea kujitokeza kujiandikisha.
Amesema makundi mbalimbali yemefikiwa na elimu hii na Sasa muamko ni mkubwa hasa vijana na wanawake wanaonekana kuhamasika zaidi na kuendelea kujiandikisha kwa Kasi kubwa.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakari Asenga amesema zoezi hili ni muhimu kwani viongozi wanaochaguliwa ndio wasimamizi wakuu wa mradi ya maendeleo Ngazi ya Vitongoji na vijiji.
Anasema wananchi wanatakiwa kujitokeza Ili kuwa na sifa ya kupiga kura novemba 27 kwenye uchaguzi Ili kupata kiongozi ambaye anaweza kusukuma gurudumu la maendeleo.
Nao baadhi ya wakazi wa Mji huo wamesema hamasa inayotolewa na viongozi wa Halmashauri hiyo imechochea Watu kujitokeza Kwa wingi kwani uelewa umeongezeka zaidi.