Wanafunzi kutoka vyuo Mbali Mbali nchini wamejitokeza kwa wingi katika studio za Producer S2kzy kwa lengo ka kurecord nyimbo zao na hii ni baada ya producer huyo kutangaza kuwafanyia wanafunzi production ya kurecord nyimbo bure kabisa bila kulipia chochote
S2kzy (Zombie) ameiambia AyoTV kuwa zaidi ya wanafunzi 160 walifika siku ya Jana kwaajili ya kurecord na wengine walilazimika kulala hapo hapo studio kwa nje ili waweze kutimiza ndoto zao za kurecord na producer huyo mwenye hit song za kutosha kwa sasa
“Watu wamekuja wengi sana kijiji kama chote watu walikuwa wanakaribia 200 na hao wengine wamelala chini alfajiri ya saa 10 wakisubiri kurecord” S2kyz
Wiki iliyopita producer S2kyz alitangaza kufanya production ya Kurecord audio bure kwa wanafunzi tu haswa mwanafunzi yoyote atakayeenda na kitambulisho atarekodiwa bure kabisa zoezi ambalo limeanza jumatatu ya Jana na litakuwa la wiki moja..
#millardayoENT