Kampuni ya Google imetia saini mkataba wa kwanza duniani wa kununua nishati kutoka katika vinu vidogo vya nyuklia ili kuzalisha nishati inayohitajika kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya akili bandia (AI).
Kampuni hiyo imeagiza vinu takribani saba vidogo vya nyuklia (SMRs) kutoka katika mtambo wa Kairos Power ya California, awamu ya kwanza ambayo itakamilika ifikapo mwaka 2030 na iliyosalia ifikapo mwaka 2035.
Vinu hivyo vitatoa suluhisho la umeme na kukidhi mahitaji ya vifaa vinavyohitaji kiwango kikubwa cha umeme kama vile AI Generative na programu nyingine ambazo zimeongeza kiwango cha matumizi ya umeme.
Ikumbukwe kuwa Kampuni ya Microsoft mwezi uliopita ilifanya makubaliano ya kuchukua nishati kutoka katika kinu cha Three Mile Island ili kuwezesha mitambo yake kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano.