Mahakama nchini Kenya inatarajiwa hii leo kutoa uamuzi wake katika kesi inayolenga kulizuia bunge la senate kujadili na kupiga kura kuhusiana na mswada unaolenga kumtimua naibu wa rais Rigathi Gachagua
Katika tukio la kihistoria wiki iliopita, bunge la kitaifa lilipiga kura kumtimua Gachagua anayekabiliwa na makosa 11 ikiwemo ufisadi.
Gachagua mwenye umri wa miaka 59 amekanusha madai yote na kwa sasa ataendelea kuhudumu katika wadhifa wake hadi pale ambapo bunge la senate litaidhinisha kutimuliwa kwake.
Naibu huyo wa rais aliwasilisha kesi mahakamani akitaka bunge la Senate kujadili mswada huo siku ya Jumatano na Alhamis, akidai kwamba mpango huo haukufuata sheria na ulifanywa kwa haraka bila ya kuzingatia matakwa yote.