Kylian Mbappe amekanusha madai dhidi yake kuwa ni “habari za uongo” baada ya polisi wa Uswidi kuanza uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji kumuhusu.
Gazeti la Uswidi Expressen liliripoti kwamba mshambuliaji huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 25 ndiye mshukiwa kufuatia tukio lililotokea katikati mwa jiji la Stockholm.
Aftonbladet lilikuwa ni chapisho la kwanza kusema kwamba madai ya ubakaji yameripotiwa kwa polisi, lakini hawakumtaja mtuhumiwa.
Mamlaka ya Mashtaka ya Uswidi ilisema katika taarifa yake: “Kwa kujibu ripoti za vyombo vya habari kuhusu tuhuma za ubakaji huko Stockholm, mwendesha mashtaka anaweza kuthibitisha kwamba ripoti ya jinai imewasilishwa kwa polisi.
Kulingana na ripoti hiyo, tukio hilo lilitokea Oktoba 10 saa hoteli katikati mwa Stockholm.” Mamlaka hiyo haikumtaja mtuhumiwa.
Mbappe hakuchaguliwa kwenye michuano ya kimataifa ya Ufaransa ya Oktoba mwaka huu alipokuwa akirejea katika hali yake ya utimamu wa mwili kutokana na jeraha la misuli ya paja na alitembelea mji mkuu wa Uswidi na kundi la marafiki zake Alhamisi, Oktoba 10.