Mkali wa muziki wa hip-hop Sean ‘Diddy’ Combs anatazamiwa kusalia gerezani huku mahakama ya rufaa ikijadili iwapo anafaa kupewa dhamana.
Rapa huyo amekuwa akizuiliwa katika gereza la Metropolitan Detention Center huko Brooklyn tangu kukamatwa kwake, huku jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Pili ya Rufaa ikizingatia ombi la timu yake ya kisheria kuachiliwa.
Siku ya Ijumaa, Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Shirikisho William J. Nardini alikataa ombi la Combs kuachiliwa mara moja, ikisubiri uamuzi wa jopo la majaji watatu. Hii ina maana kwamba Combs ataendelea kukaa katika jela ya Brooklyn huku mahakama ikitathmini rufaa ya mawakili wake.
Hakimu pia aliruhusu timu ya wanasheria ya Combs kuwasilisha ombi lao la dhamana chini ya muhuri na marekebisho ya sehemu, kuhakikisha baadhi ya maelezo ya kesi yanabaki kuwa siri.